Rafiki Mupotevu


Rafiki
July 12, 2008, 1:00 pm
Filed under: Uncategorized

Nilikuwa na rafiki yangu tuliyependana naye sana. Rafiki yangu alitoweka na kuniacha pekee yangu bila chochote.

Nilikasirika sana kwa sababu alinitoroka. Nilijaribu kumtafuta lakini sikumpata. Nilienda kwa wavyele wake,lakini swala iliyotoka vinywani mwao kabla sijaulizia hali ya mwenzangu, ilikuwa ni,”Unajua mwenzako aliko?”

Nilipowajibu kwamba sijampata, nyuso zao zilijawa na huzuni. Kisha, mamake akanishawishi nisiwe kama mwanawe, kwa vile alikuwa amezungumza naye ya kutosha, lakini hayo yote yaliambulia patupu. Mamake alikuwa amempenda kumpenda lakini hayo yote, hayakuwa kitu kwake.

Baadaye, nilikuja kujua kwamba, kutoweka kwa rafiki yangu ilikuwa baada ya kupata vitisho kutoka kwa babake kwamba  atamcharaza viboko. Kisha naye, akaamua kutoweka ili atoroke hayo viboko. Baadaye, ikawa uchungu kwa wavyele wake. Mamake alikata roho mwaka uliopita, kisha babake akafuatia mwaka huu. Wakifa, bado walikuwa na uchungu nyoyoni zao, wapi watampata mwanao.

Waliacha watoto mayatima, wakiwa maskini hohe hahe, hawana chochote. Tegemeo lao ni marafiki na majirani ambao huwasaidia na hela kidogo ya mahitaji zao.

Ni ombi langu kuwa, rafiki yangu atarejea nyumbani siku moja ili awashughulikie wenzake. Nawaza na kuwazua wakati ninake alikuwa anaugua, mimi ndiye nilikuwa namshughulikia kwa vile alikuwa hajiwezi kabisaaaaaaaa.Wanawe nao walikuwa bado wachanga. Kwa sasa, sijui anayewashughulikia ni nani.

Kila ninapopiga darubini juu ya rafiki yangu, mimi hushikwa na huzuni mno, huku natiririkwa na machozi yasiyoweza kufutika.

Tafadhali, njoo…..rafiki….njoo.

Translation

Friend

I had a friend and we loved each other very much. My friend left me alone without anything.

I was annoyed because my friend ran away and I tried to find her but I couldn’t. I went to my friend’s parents and they asked me where my friend was. I told them that I could not find her. My friend’s mother told me not to be like my friend, Hellen. We searched a lot for my friend. Her mother said “my daughter, my daughter, I don’t know what to do since I don’t know where you are.” I said, “it’s okay.” Her mother looked at me then said, “I was not like that, I was trying to love my child. She doesn’t need her mother.”

Before Hellen ran away, her father had said that he would beat her very bad. This is why she ran away. He mother searched for her but she could not find her. Still, we are searching for her. Her mother died last year, and her father died before that. My friend’s brothers and sisters were taken back to their rural home. My family is sending them money for spending and for school fees.

My friend is very bad, I don’t know why she did that. My friends are suffering, when I find Hellen, I will be very happy because she will help them. I don’t know what to say because I have been shocked since the time she ran away. I was very sad. Hellen’s mother got very sick and she didn’t find anyone to help her except for me. I helped her do her chores around the house. Now my friend doesn’t have a mother or a father. Her siblings are orphans, they don’t have enough food and they are being helped by others to get food. I feel very bad since her parents died since her siblings keep on begging.

Advertisements